UPANGAJI UZAZI NI MUHIMU

C2

Upangaji uzazi ni suala nyeti ambalo nia yake ni kuthibiti idadi ya watu nchini na kote ulimwenguni.Mtu mzima ambaye ana uwezo wa kuzaa inafaa azae watoto anaweza kimu mahitaji yao ya kimsingi hadi pale wanaweza kujitegemea  maishani.lakini hili limeonekana kinyume.Kwa mujibu na mila na tamaduni za kiafrika na kasumba ambazo zimepitwa na wakati,zinadokeza kuwa kuzaa watoto wengi ni jambo ambalo linampa mwanamume hadhi katika jamii husika.Swali ambalo tunapaswa kujiuliza ni mbona uzae watoto  ambao huwezi kulea?

C1 C4

Wengi hawajakubali ukweli kuwa kuzaa  si kazi kazi ni kulea.Hivyo kuna haja ya mashirika husika na washika dau katka uthibiti wa idadi ya watu ulimwenguni kujitokeza  na kuwaelimisha wananchi watu wazima njia za kupanga uzazi na idadi  bora ya kupata watoto ili kupunguza idadi ya watoto ambao wametelekezwa na kuishia kurandaranda mijini kuombaomba ili kutia kitu mdomoni.

Motto ni Baraka kutoka kwa maulana hivyo basi hakuna haja kutesa viumbe hivi  visivyo na hatia baada ya kutua duniani na kurambishwa shubiri badala ya asali.

Serikali pia inafaa kubuni mradi wa kufadhili mahitaji ya watoto wawili  kama matibabu,elimu na lishe katika kila familia kusaidia katika kuthibiti hali ya kuzaliwa watoto wengi katika jamii yetu.

Advertisements
By The VOICE

UNUNUZI WA VIPAKATALISHI NI MUHIMU

Kutupiliwa mbali kwa zabuni ya mradi wa vipakatalishi kwa watoto wa darasa la kwanza ni hatua mbaya ambayo italemaza  uwezo wa chipukizi hawa kukua kiteknolojia.Ikizingatiwa ya kwamba watoto hawa ndio viongozi wa kesho kwa mtazamo wa wanajamii ambao huamini kuwa kesho ni ya  wanaozaliwa.Ukweli ni kuwa karne hii inakuwa kwa kasi zaidi kwa kuzinduliwa kwa vyombo vipya vya kidigitali kama rununu za kutomasa,tarakilishi,vipakatalishi na vyombo vya uhandisi na vya habari ambavyo ni bora zaidi ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

L

Ni bayana kuwa matumaini yao yameponzwa na kiu yao kukosa  ‘maji’ ya kukikata.Ni hatua ambayo imeonyesha ubutu wa ahadi za serikali ya Jubilee ilizotoa katika manifesto yao wakati wa  kampeni za uchaguzi  mkuu uliopita.Iwapo serikali haitachukua hatua za matendo kutimiza mpango huu,huenda viongozi wa upinzani wakapata uungwaji mkono na wakenya  kushinikiza serikali na kutimiza ajenda ya kura ya maamuzi.

Hususan katika harakati za kuafikia malengo ya ruwaza ya mwaka wa 2030 ni pigo katika sekta ya teknolojia na mawasiliano  muundo msingi ambao sasa utachukua muda kusuluhisha ikizingatia kuwa siasa chafu zitaanza kuchezwa na viongozi wetu kuhusu mradi huu.

Ilivyo desturi ahadi ni ni deni na dawa ya deni ni kulipa.hivyo basi serikali ina jukumu la kutekeleza kupitia wizara ya elimu ambayo iko chini ya himaya ya profesa Jacob Kaimenyi ili kuwapa wananchi imani  kuwa serikali ina uwezo wa kuwasaidia kupitia kwa miradi mbalimbali.

By The VOICE

SUDAN KUSINI YAHITAJI NCHI ZINGINE KUKUA KIUCHUMI

Suala la kutimua wafanyakazi wa kigeni katika nchi ya Sudan kusini ni hatua ambayo italemaza ukuaji wa uchumi  wa nchi hiyo changa  katika bara la Afrika.Ni jambo la kushangaza kuona nchi changa mno kujitenga na nchi zingine kama Kenya ambazo zimetoa msaada na mchango mkubwa kwa  Sudan Kusini kujisimamia na pia kuwapa hifadhi wakimbizi makaazi katika kambi za humu nchini.

SUDAN KUSINI

Agizo la kuwafukuza wafanyakazi wa kigeni na kampuni na pia mashirika ya kibinafsi  yatapelekea nchi husika kukoma kutoa msaada wowote na pia kuwarudisha wananchi wa Sudan Kusini nchini mwao walio humu nchini.

Ikizingatiwa ya kuwa Kenya imekuwa mshirika wa karibu wan chi hii kwa miaka mingi,nchi hiyo  chini ya uongozi wa Rais Salva Kiir hawajaona mchango na sasa ni bayana kuwa asante ya punda ni mateke.

Kwa maoni  yangu  Sudan Kusini haijafikia kiwango cha kujisimamia bila kutegemea nchi  jirani  kama Kenya,Uganda,Ethiopia na ndugu  yao Sudan  kwa  sababu wafanyikazi wao wana ujuzi na tajriba kutoka nchi zao ambazo zimepiga hatua kimaendeleo.

images (5)

By The VOICE

PENZI LAHITAJI WAWILI WAPENDANAO-UTAMU WA MAHABA

Mapenzi huwa matamu kwa wawili walio na hisia moja ya kimwili na kimafikira kwa mwenzake.wawili wanapokata kauli kupendana changamoto na mafanikio ushuhudiwa katika safari hii inayoonekana kuwa ngumu kwa asiye na subira na uvumilivu.

images (1)

Ili penzi kunoga na kushamiri virutubisho muhimu kama uvumilivu,uaminifu,heshima,maelewano,kujitolea ,maombi ya maongozi kutoka kwa mola na ukakamavu huwa muhimu katika kutunza na kulea penzi changa.

Mambo mengine yanayotia penzi ladha ni,kuzuru  vituo vya burudani kujiliwaza,vivutio tulivu kujadili mambo muhimu katika penzi lao,pesa na kununuliana zawadi huchangia pakubwa kuzidisha mapenzi.

Penzi lisipotunzwa huporomoka na linaweza pekea mmoja wa wapenzi kujitia kitanzi kutokana na kutoaminiana kwa kuwa na mipango ya kando.hivyo basi wapenzi wa jukumu la kushirikiana kutunza na kulea penzi na ndipo wahenga hawakuboronga waliponena kwa methali,kichango ni kuchangizana.

download

images

@jmediaservicesJOASH ONSARE

By The VOICE

KENYANS AVOID CRIME AND ACCIDENT SCENES

Camping of people in accidents and terrorist affected areas has been witnessed day in day out. The posed danger by these  big crowds who seem to be ignorant  and driven by curiosity, forget that terrorist target a multitude of people to achieve their ill motive missions.

In regard to the continuous occurrence of this incidences of bombing the government has tried to sensitize Kenyans to be  vigilant in avoiding places where there are many people who are seemingly hotspots of terrorists, also accidents have been occurring too but the culture of people gathering  on the scenes remains evident. The question we  ask, When will we learn not to appear near crime and accident scenes? It looks like Kenyans don’t understand the areas not to be close to, which might cost their life. Therefore  the government should come up with more programs on radio, Television and newspapers and free journals that will equip people with knowledge on how to be safe especially in evading crime and accident scenes.

The  road accidents that occur continuously in Salgaa  is an example of one among many where Kenyans gather to witness and sometimes siphon oil from tankers and harvest maize grains that they never sow hence claiming their lives directly and indirectly.Other incidences where people have been seen crowded include the coast region, blast on Thika super highway and the most current blast at Gikomba open air market that claimed about 10 lives and more than 70 left injured.

Every creature has a right to live, so its our responsibility to ensure we are careful in every step we make, not to risk to places that are a threat. Also we should ensure we maintain our security and inform the police on suspicious elements among us.

 

By The VOICE

UWEPO WA USALAMA NI WAJIBU WA KILA MTU

Swala la ukosefu wa usalama nchini limeonekana kuwa donda ndugu ambalo halina tiba mwafaka.Haya yamedhihirika wazi kutokana na vitendo vya ugaidi vinavyoshuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini kama mkoa wa pwani,Nairobi na mkoa wa kaskazini mashariki.Ili kumbukumbu hizi za ugaidi ziwepo siku zijazo taswira itakoyorejelewa ni ile ya mtoto Satrin Osinya kujeruiwa na mamake kuuawa katika shambulizi lililotekelezwa likoni,Mombasa.

Ili kupunguza na kumaliza viza hivi ambavyo vinatokea mara kwa mara nakuangamiza na kujeruhi watu wasio na hatia,mimi wewe na serikali ,lazima tuwajibikie usalama kabla serikali haijaingilia kati kwa sababu sisi ndio tunawajua tunaoishi nao ata kabla serikali haijawatambua.

Ni vyema kila mtu ambaye anashuhudia kisa kisicho cha kawaida ama mtu ambaye unamshuku kuripoti katika kituo cha polisi kilicho karibu nawe.pia serikali inafaa kuajiri maafisa wa polisi kwa wingi,kuwapa silaha za kisasa na mafunzo mapya ili kukabiliana na kuzuia visa hivi hatari kwa binadamu.

 

By The VOICE