Quote

Mapungufu maishani na pia changamoto humfanya binadamu kutia bidii katika kila jambo alifanyalo.Bila motisha haya hayawezi afikiwa.
Ni vipi tutahakikisha changamo tumezipunguza katika kila tunalofanya?TOA MAONI YAKO….

Joash Onsare

JINSI YA KUKABILI CHANGAMOTO

By mzingaleo

MAGAIDI WANAOJISALIMISHA WAONGEZWE MUDA

Makataa ya  siku kumi kwa vijana wakenya waliojiunga na kundi la kigaidi kujisalimisha ili kusamehewa  ni hatua nzuri ambayo inanuiwa kuleta hadhi ya kenya haswa katika idara ya usalama.
Haya yote yanapotarajiwa,njia na taratibu mwafaka zinapaswa kuweka ili kuhakisha wahusika wamepewa mafunzo ya jinsi ya kutafuta riziki kwa kutumia njia mbadala isiyoponza mwananchi yeyote ama maendeleo  nchini.
Pia serikali inapaswa kuwapa vijana hao siku zisizozidi 30 ili wajisalishe kikamilifu kwa serikali na kufanikisha hil, viongozi wa kidinina na masheikh wapewe jukumu kuwapeleka wahusika katika vituo vya polisi .
Hatua hii ikitimia kenya itakuwa imepiga hatua katika kupambana na ugaidi umbao umekuwa kero nchini.

By mzingaleo

WANAFUNZI VYUONI WAPOTOKA

NA DENNIS MURITHI

Wanafunzi wa vyuo vikuu humu nchini husema kuwa wanafurahia maisha ya shule kwani huwa hawanyimwi ruhusa ya kutenda jambo lolote wanalofikiria linawapendeza. Hapo ndipo utapata ya kwamba wengi wao wanajiingiza katika maisha ya anasa na kusahau kilichowaleta chuoni. Hata kama ni vigumu kwa walimu wao kuwarekebisha, ni vyema wawafanyie mafunzo na maelekezi ya jinsi wanavyofaa kuwa na maadili na kuachana na tabia duni ambazo hatimaye zinawadhuru katika siku za halafu.

31

tusije tukawalaumu chipukizi hawa pekee,wazazi wao pia walifeli katika kuwaelekeza wanachostahili kufanya katika mazingira mbalimbali.ndipo wahenga waliponena bila kukosea asiyefunzwa na ulimwengu hunzwa na ulimwengu.

By mzingaleo

KIPINDI CHA MAJARIBU ‘MY DRESS MY CHOICE’

NA RAPHAEL GITAU
Kutokana na tukio lile la mwanamke aliyevuliwa nguo jijini Nairobi wiki mbili zilizopita, Wanawake wamekuwa na vioja vingi sana tangu huo wakati kwani wengine wao wameamua kwenda hata wakiwa uchi wa mnyama.
m2
Mazungumzo yake Makamu wa Rais Arap Samoei Ruto yaliwavutia na kuwashika pema kwani alikuwa kwa upande wao. Si ajabu sana kuwaona wengine wao wakitembea na mavazi mawili tu, moja yazo ikiwa ni nguo ya ndani moja tu na kumalizia na kanchiri na ukimwona barabarani ako raha mstarehe kabisa huku maozi yote yakimkondolea macho. Jambo hili limekidhiri sana humu upande wa Thika na jijini Nairobi bila kuacha vijiji vingine vikubwa humu nchini. Kwa kweli hili jambo linakera sana wazazi wakiwaona watoto wao wakitembea uchi. Ningeomba serikali iingilie kati na ifuatilie nyayo za Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwamba watu wavalie mavazi yaliyo na heshima na taadhima. Hapo ndipo sisi wenyewe kama wakenya na vijana wetu wataweza kukua wakiwa na adabu na kuifanya Kenya kuwa makaazi mazuri ya kuishi.

By mzingaleo

FUNUNU ZISIZO NA MSINGI ZIKOMESHWE

NA DENNIS MURITHI,THIKA

Kutokana na visa vya ugaidi vinavyotokea humu nchini kila kuchao, lawama zimeonekana kuelekezwa kwa kundi haramu la Alshabaab. Huku  sifa zikienezwa kote kuwa hili kundi ndilo limetenda hayo maasi hata ingawa si wao wametenda. Kusema kweli wakati hili kundi haramu linasikia vyenye sifa zao zimeenezwa, huwa ndiyo  furaha kubwa kwao wakati watu wengine wanaomboleza vifo vya wapendwa wao na mali ya mamilioni kuibwa na kuharibiwa. Kwa hivyo, tunawaomba wanaoeneza sifa duni za hawa mashetani watu wakome ili kutowafanya watu kuhofia maisha yao wanakoishi.

NNNN TTTT

Pia katika harakati za kupunguza visa hivi kila mtu ana jukumu la kutekeleza kwa kuhakikisha kuna usalamu humu nchini

By mzingaleo

TUEPUKANE NA WAHUBIRI GHUSHI

images

Visa vya wahubiri kuvuna wasikopanda kuendelea kunoga katika vinywa vya wengi ni ishara tosha kuwa ulimwengu uko katika siku za mwisho zilizotabiriwa katika maandiko matakatifu.Ni dhahiri shahiri kuwa watu wamejificha kanisani ili kutekeleza maovu kama utapeli,ukahaba,wizi,mauji ya wenzao.Huku sura tunayovalia nje ikiwa  tofauti  na yenye iko ndani mwetu.waswahili hawakukosea waliponena tenda wema nenda zako na bila shaka wema utakufuata.

download (1)  download

Viongozi ni vielelezo wa kuigwa katika nyanja mbalimbali lakini ni kinyume na baadhi ya viongozi wa makanisa ambao wameonekana kutenda dhambi kwa waumini wao.Wakati msasi anawageuka kondoo wake na kuanza kuwadhulumu na kuwala thibitisho kuwa wakufa na hawataweza kukuwa kiroho na badala yake kutoroka kanisani wakiogopa kupotoshwa na mapasta ghushi wema tamaa ya kula vya bwerere.
Serikali inapaswa kuwafanyia uchunguzi wahubiri kama hawa na kuonya umma na huduma  kuhusu zao.pia waumini inafaa wawe macho na kuamini mungu na si binadamu ili kuzuia kuadaiwa na hawa matapeli wanavalia ngozi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu.
By mzingaleo

UPANGAJI UZAZI NI MUHIMU

C2

Upangaji uzazi ni suala nyeti ambalo nia yake ni kuthibiti idadi ya watu nchini na kote ulimwenguni.Mtu mzima ambaye ana uwezo wa kuzaa inafaa azae watoto anaweza kimu mahitaji yao ya kimsingi hadi pale wanaweza kujitegemea  maishani.lakini hili limeonekana kinyume.Kwa mujibu na mila na tamaduni za kiafrika na kasumba ambazo zimepitwa na wakati,zinadokeza kuwa kuzaa watoto wengi ni jambo ambalo linampa mwanamume hadhi katika jamii husika.Swali ambalo tunapaswa kujiuliza ni mbona uzae watoto  ambao huwezi kulea?

C1 C4

Wengi hawajakubali ukweli kuwa kuzaa  si kazi kazi ni kulea.Hivyo kuna haja ya mashirika husika na washika dau katka uthibiti wa idadi ya watu ulimwenguni kujitokeza  na kuwaelimisha wananchi watu wazima njia za kupanga uzazi na idadi  bora ya kupata watoto ili kupunguza idadi ya watoto ambao wametelekezwa na kuishia kurandaranda mijini kuombaomba ili kutia kitu mdomoni.

Motto ni Baraka kutoka kwa maulana hivyo basi hakuna haja kutesa viumbe hivi  visivyo na hatia baada ya kutua duniani na kurambishwa shubiri badala ya asali.

Serikali pia inafaa kubuni mradi wa kufadhili mahitaji ya watoto wawili  kama matibabu,elimu na lishe katika kila familia kusaidia katika kuthibiti hali ya kuzaliwa watoto wengi katika jamii yetu.

By mzingaleo

UNUNUZI WA VIPAKATALISHI NI MUHIMU

Kutupiliwa mbali kwa zabuni ya mradi wa vipakatalishi kwa watoto wa darasa la kwanza ni hatua mbaya ambayo italemaza  uwezo wa chipukizi hawa kukua kiteknolojia.Ikizingatiwa ya kwamba watoto hawa ndio viongozi wa kesho kwa mtazamo wa wanajamii ambao huamini kuwa kesho ni ya  wanaozaliwa.Ukweli ni kuwa karne hii inakuwa kwa kasi zaidi kwa kuzinduliwa kwa vyombo vipya vya kidigitali kama rununu za kutomasa,tarakilishi,vipakatalishi na vyombo vya uhandisi na vya habari ambavyo ni bora zaidi ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

L

Ni bayana kuwa matumaini yao yameponzwa na kiu yao kukosa  ‘maji’ ya kukikata.Ni hatua ambayo imeonyesha ubutu wa ahadi za serikali ya Jubilee ilizotoa katika manifesto yao wakati wa  kampeni za uchaguzi  mkuu uliopita.Iwapo serikali haitachukua hatua za matendo kutimiza mpango huu,huenda viongozi wa upinzani wakapata uungwaji mkono na wakenya  kushinikiza serikali na kutimiza ajenda ya kura ya maamuzi.

Hususan katika harakati za kuafikia malengo ya ruwaza ya mwaka wa 2030 ni pigo katika sekta ya teknolojia na mawasiliano  muundo msingi ambao sasa utachukua muda kusuluhisha ikizingatia kuwa siasa chafu zitaanza kuchezwa na viongozi wetu kuhusu mradi huu.

Ilivyo desturi ahadi ni ni deni na dawa ya deni ni kulipa.hivyo basi serikali ina jukumu la kutekeleza kupitia wizara ya elimu ambayo iko chini ya himaya ya profesa Jacob Kaimenyi ili kuwapa wananchi imani  kuwa serikali ina uwezo wa kuwasaidia kupitia kwa miradi mbalimbali.

By mzingaleo

SOKO LA HISA

SARAFU                                           KUNUNUA                                     KUUZA

Dola ya Marekani                                   85.39                                                    85.29

Pauni 1 ya Uingereza                            128.23                                                  128.10

Euro 1 ya Ulaya                                     109.71                                                  109.57

Shillingi 1 ya Kenya/USHS                     30.55                                                    30.45

Shillingi 1 ya Kenya/TSHS                     19.22                                                    19.14

  Kwa hisani ya CBK 

By mzingaleo

SUDAN KUSINI YAHITAJI NCHI ZINGINE KUKUA KIUCHUMI

Suala la kutimua wafanyakazi wa kigeni katika nchi ya Sudan kusini ni hatua ambayo italemaza ukuaji wa uchumi  wa nchi hiyo changa  katika bara la Afrika.Ni jambo la kushangaza kuona nchi changa mno kujitenga na nchi zingine kama Kenya ambazo zimetoa msaada na mchango mkubwa kwa  Sudan Kusini kujisimamia na pia kuwapa hifadhi wakimbizi makaazi katika kambi za humu nchini.

SUDAN KUSINI

Agizo la kuwafukuza wafanyakazi wa kigeni na kampuni na pia mashirika ya kibinafsi  yatapelekea nchi husika kukoma kutoa msaada wowote na pia kuwarudisha wananchi wa Sudan Kusini nchini mwao walio humu nchini.

Ikizingatiwa ya kuwa Kenya imekuwa mshirika wa karibu wan chi hii kwa miaka mingi,nchi hiyo  chini ya uongozi wa Rais Salva Kiir hawajaona mchango na sasa ni bayana kuwa asante ya punda ni mateke.

Kwa maoni  yangu  Sudan Kusini haijafikia kiwango cha kujisimamia bila kutegemea nchi  jirani  kama Kenya,Uganda,Ethiopia na ndugu  yao Sudan  kwa  sababu wafanyikazi wao wana ujuzi na tajriba kutoka nchi zao ambazo zimepiga hatua kimaendeleo.

images (5)

By mzingaleo